Wananchi wa kata ya Nzera iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita wameanza kunufaika na Mradi wa Maji safi na salama ulipo katika kijiji cha Nzera.
Meneja wa Wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini Ruwasa Mkoa wa Geita Mhandisi Jabiri Kayilla amesema mradi huo unatekelezwa kwa fedha za Mpango wa mapambano dhidi ya UVIKO 19 ambapo Mkoa wa Geita ulipokea bilioni 2.4 kwa ajiri ya utelekelezaji wa Miradi ya maji katika Mkoa.
Mhandisi Kayilla amesema wananchi wa Nzera wanakwenda kunufaika na Mradi huo wa maji kwa kuwaondolea changamoto ya kufata maji umbali mrefu.
Kayilla amewataka wananchi ambapo miradi hii unatekelezwa kuhakikisha kwamba wanakuwa walinzi wa kuilinda miradi hiyo ili iweze kutumika kwa mda mrefu pamoja na kuchangia huduma ya maji kuwezesha miradi hiyo kuwa endelevu.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Geita Mhandisi Sande Batakanwa amesema mradi huo unahusisha ujenzi wa tenki lenye ujazo wa Lita 100,000, ujenzi wa vituo 7 Vya kuchotea maji ambapo vijiji viwili vya Nzera na Bugando vitanufaika na mradi huo.
Mhandisi Sande amesema mradi huo umetengewe kiasi cha milioni 361.7 huku mpaka sasa wameshatumia milioni 285.69 na umefikia asilimia 98 huku wanufaika wa mradi huo ni zaidi ya wananchi 6,787 ambapo mpaka sasa wameshaanza kupata huduma ya maji safi na salama.
Comments
Post a Comment