SERIKALI IMEWATAKA WAMIlIKI WA LESENI KUJIANDA KIMKAKATI


Waziri wa madini Tanzania Dkt. Doto Biteko amewataka wamiliki wa Leseni za Madini kujipanga kufanya kazi zao kimkakati ili kuwana uzarishaji bora wa madini mbalimbali yakiwemo ya dhahabu.

Dkt Biteko amesema Serikali ilivyojiandaa GST kufanya tafiti za Kina kwa kushirikiana na wamiliki wa leseni.

Asema licha ya mikakati hiyo Wizara inatoa nafasi kubwa kuwasikiliza na kushauriana na wadau wa madini haliambayo otaleta y8ja kwa wachimbaji. 

Waziri wa madini alilani vitendo vinavyo fanywa na baadhi ya wa fanyabiashara wa madini wanaochukua fedha kwa wageni wanao kuja kwa lengo la kuwekeza huo niwizi vyombo vya dola vitashughulika nao.

"Tanzania ina utajiri  mkubwa wa rasilimali madini, Tuna aina zaidi ya 100 za Madini ya Vito yanayochimbwa, Tuna madini yanayotumika viwandani, madini kwa ajili ujenzi, chumvi kama chakula, tuna metali na mengine mengi," amesema Dkt Biteko na kuongeza kuwa.

"Nchi yetu imefunguka kwa kiasi kikubwa kiuwekezaji,  Kwenye madini ya kimkakati tunafanya tafiti mbalimbali, Gesi adhimu ya Helium inafanyiwa utafiti, madini ya nikeli yanafanyiwa utafiti, jotoardhi inafanyiwa utafiti na madini mengine," amesema Dkt Biteko.

Amesema sio kwamba tumeharakishwa bali inatokana na mahitaji ya dunia,  Tayari tunao mkakati wa kuyatafiti kujua yako wapi kwa kiasi gani, tutajenga viwanda vyetu kuyachakata hapa hapa nchini.

Waziri Dkt Biteko amesema Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ilikuwa inafanya tafiti za awali, tumebadili  Sheria imepewa nguvu kufanya tafiti za kina.

Amesma GST tumeipa fedha kupeleka huduma za kimaabara kwa jamii, Tayari tumejenga ofisi Mkoani Geita tutajenga Chunya na maeneo mengine.

Muda si mrefu dhahabu isiyosafishwa haitaruhusiwa kwenda nje Taratibu za Kiserikali zitakapokamilika tutaanzisha utaratibu mzuri ikiwa hivi sasa  Benki Kuu ya Tanzania imeanza kununua dhahabu yetu.

Alitaja Changamoto kubwa inayoikabili Sekta ya Madini ni watu kuchanganya haki ya  Ardhi na haki ya Madini, Wamiliki wa ardhi watoe haki kwa wamiliki wa haki madini kwa makubaliano ya kishwria.

Dkt Biteko ameswma Wizara ya Madini ni Wizara inayofanya sana mashauriano na wadau, nia ni kusikilizana na kukubariana Maboresho ya Sheria na Kanuni tuliyofanya  yametokana na mashauriano ya wadau.

Nakwamba Wazawa kwenye Sekta ya Madini wamepewa nguvu kubwa sana, Kwenye  madini ya tanzanite tumetoa fursa kwa wazawa ikiwa Leseni ndogo wamepewa wazawa.

Dkt Biteko amesema Mhe.  Rais Samia Suluhu Hassan anaiangalia Sekta ya Madini kwa kipindi kirefu kijacho  haangalii miaka 10 ijayo na kwamba Tuna bahati kimkakati nchi yetu ipo vizuri, ipo vizuri kijiografia na miundombinu kama  ujenzi wa reli ya SGR, barabara, viwanja vya ndege pia nchi yetu ina amani.

Waziri wa madini alowaonya  wafanyabiashara  wasio waaminifu kuacha kutumia leseni zao za biashara ya madini kuibia wageni serikali kupitia wizara ya madini haita kubari Leseni kuchafua taswira ya nchi.


 Amesema Sekta ya Madini imekua kivutio na inavutia watu wengi na Zaidi ya leseni 300 za uchimbaji wa Kati ni za wazawa na zaidi ya leseni elfu 30 ni za uchimbaji mdogo.

Comments