MWENYEKITI WA KITONGOJI AVULIWA UANACHAMA NA UMWENYEKITI KWA TUHUMA ZA KUOMBA FEDHA KWA WALENGWA WA TASAF.


 Mwenyekiti wa kitongoji cha Misiri kilichoko Kijiji cha Isemabuna kata ya Butinzya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita Lazaro Igulyati  amevuliwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi na uongozi wa tawi la Cha hicho Isemabuna kwa tuhuma ya kutokuwa na nidhamu kwa viongozi wa chama  hicho wanapomuita kwenye vikao anakuja amelewa huku akitoa lugha chafu  huku wakimtuhumu pia kuwaomba fedha walengwa wa TASAF.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Tawi la CCM Isemabuna Msafiri Emmanuel wakati akizungumza na Blog ya Bukombesasa kwa njia ya simu alisema kamati ya siasa ilifikia uamzi huo Februari 3, 2023 baada ya kumuita mara kadha kwa ajili ya kuonywa ili kuacha tabia hizo na amekua akirudia likiwemo la kuwaomba Tsh10000 hadi sh 20000  walengwa wa kaya masikini huku akijua fedha hizo ni za mashariti ya Tasaf.

Aidha Emmanuel alisema licha ya kukili kutenda makosa hayo kamati ya siasa ilimtaka kusoma mapato na matumizi tangu awekwe kwenye nafasi hiyo hajawahi kusoma mapato na matumizi.

Katibu CCM kata ya Butinzya Boniphace Sahani amekili kupokea mazimio ya kikao ngazi ya tawi ya kuvuliwa uanachana na uongozi mwenyekiti huyo kwakupatikana na kosa la Kutokuwa na nizamu kwa viongozi wa chama na kuchukua fedha za walengwa wa Tasaf hivyo tutalifanyia kazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM kata ya Butinzya Said Kwangu alisema taarifa amezipokea ofisini kwake za mwenyekiti huyo wa kitongoji ana utovu wanidhamu na kuongea kuwa kosa hilo sio la kwanza licha ya kuonywa na chama hali ambayo imepelekea kuvuliwa uanachama.

Kwangu alisema mwenyekiti wakitongoji alikuwa anawafatili walegwa waTASAF  akiwatishia kuwafuta kwenye TASAF kwasababu wanapokea fedha hawampi chochote huku aliwapambania kuwaweka kwenye TASAFna walegwa walikuwa wanampa kuazia sh 5000 na kuendelea wakihofia kufutwa.

Mwenyekiti wa CCM kata alisema kutokana na kuzipokea taarifa hizo na mihitasari za vikao vya kamati ya siasa leo Februari 2,2023 anatarajia kutoa utaratibu wa chama kwa ofisa mtendajo wa kijiji cha Isemabuna amunyang'anye nyaraka za serikali ikiwemo mhuri na asiendelee na majukumu ya kiserikali kwa wananchi.

MWISHO.

Comments