Katibu Mkuu Wizara ya Madini Adolf Ndunguru ameongoza ujumbe wa Wizara na wadau wa madini kutoka Tanzania

 

Katibu Mkuu Wizara ya Madini  Adolf Ndunguru ameongoza  ujumbe wa Wizara na wadau wa madini kutoka Tanzania katika  Mkutano  wa Kimataifa wa Madini wa  Indaba unaofanyika Jijini Cape Town  nchini Afrika Kusini.

 Ambao unaenda sambamba  na maonesho  ya madini Mkutano huo unatarajiwa kuwa na manufaa makubwa kwa nchi ya Tanzania ikiwemo kuhamasisha uwekezaji kwalengo la kuongeza tija kwenye uzalishaji wa madini na kukuza Pato la Taifa.


Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Ndunguru, Kamishna wa Madini Dkt. Abdurahman Mwanga,na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt.Vanance Mwasse wamefanya mazungumzo na wawikilishi wa kampuni za madini kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Marekani na Japan kujadili  Sekta ya Madini nchini

Comments