HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOMBE YATOA MKOPO WA SH 222.2 MILIONI KWA WANAWAKE VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU
Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe imetoa mkopo wa shilingi milioni 222 kwa vikundi 35 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Ameyasema hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Lutengano Mwalwiba wakati akimkaribisha mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba kukabidhi mikopo hiyo ya bila riba zikiwemo pikipiki 20 mbuzi ijko la gesi pamoja na cherehani nne za mfano
Mwalwiba amesema Jambo hili lililo fanyika hapa limeelezwa katika ibara ya 32 na section (s) ya chama Cha Mapinduzi kuelezea kuwa kutakuwa na shughuri za uwezeshaji uchumi kwa jamii kupitia sehemu mablimbali .
Mwalwiba ameongeza kwa kusema wao Kama halimashauri wamepewa maelekeza na Sheria ya fedha ya mwaka 2018 sura namba 290 section ya 37( A)inawataka watoe asilimia 10 katika vikundi mbalimbali ili vikundi viweze kujiendeleza kiuchumi nakufikia malengo ya kwamba kila mtanzania anafurahia matunda ya Uhuru ya Nchi yetu.
Naye mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba amevipongeza vikundi kwa kuweza kupata vigezo na uhalali wa kuweza kupata mikopo kwa asilimia Mia nakuweza kuendesha miladi yao kwa kupitia mikopo hiyo na amesema katika mikopo hiyo haina riba.
Hata hivyo nkumba amevitaka vikundi vilivyopata mkopo wakati vikiendesha miladi Yao basi viweze kurudisha marejesho kwa wakati maalumu.
Afisa maendelea halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Lita Kamenya amesema fedha hizo zimetokana na mapato ya ndani ,fedha ya bakaa na fedha za marejesho ya vikundi na leo Kuna vikundi 35 kati ya vikundihivyo vikundi vya wanawake 20, vikundi vya vijana 21, na vikundi vya watu wenye ulemavu vikundi 4 .
Mwanakikundi Mahigwe Kajoro ameishukuru Serikali kwa kuweza kuwawezesha mkopo hivyo kutaweza kuwainua kiuchumi kutokana na mwanzoni alikuwa anaendesha daladala ya baisikeli na kipato chake kilikuwa shilingi 5000 kwa siku Ila kwa Sasa anamakadirio ya ya kuapata shilingi elfu 30 kwa siku
MWISHO
Comments
Post a Comment