Hali ya taharuki imezuka katika mtaa wa Fungafunga kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro baada ya Mtu mmoja mwanaume ambaye jina lake halikufahamika mara moja amekutwa mefariki huku mwili wake ukielea kwenye dimbwi la maji.
Mwenyekiti wa mtaa huo wa Fungafunga Thabiyi Mgalula amesema alipokea taarifa kutoka Kwa wananchi kua kuna mwili wa mtu ukielea kwenye dimbwi la.maji ambalo limetokana na ufatuaji matofali ndipo akatoa taarifa jeshi la Polisi na zimamoto
Kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji Emanuel Ochieng amethibitisha kutokea kwa tukio Hilo ambapo amesema Kwa sasa mwili huo utapeleka hospitli ya Rufaa Mkoa Morogoro Kwa ajili ya taratibu zingine ikiwemo uchunguzi wa Chanzo cha kifo pamoja na utambuzi.
Comments
Post a Comment