Bukombe. Wakara wa huduma za Misitu Tanzani (TFS) wametakiwa kupanda miti ya matunda kila shule ili wanafunzi wanufaike na matunda licha ya kupanda miti ya kivuli.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Yusuph Mohamed wakati wa upandaji miti 30,000 katika shule ya Sekondari Doto Biteko ikiwa ni sehemu ya shughuli zilizopangwa kufanyika kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Mohamed amesema TFS licha ya kuwa na mpango mzuri wa kupanda miti ya mbao kivuli mashuleni ni wakati wa kuona umuhimu wa kupanda miti ya matunda ikiwa kwa sasa Bukombe kunashule mpya saba zimejengwa inatakiwa zipandwe miti ya matunda
Mohamed ambae alikuwa mgeni rasmi akiongoza mamia ya wananchi, watalamu, wadau toka Taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali akiongoza zoezi hilo la upandaji miti amewataka walimu kwa kushirikiana na wanafunzi na wananchi kuhakikishe wanatunza miti hiyo na kutowaona TFS kuwa ni maadui badala yake kuendelea kuwaunga mkono.
Awali Kaimu Mhifadhi Misitu Wilaya ya Bukombe Musa Tendi akitoa taarifa ya upandaji miti amesema, "Tuendelea kutunza mazingira pamoja na hali ya tabia ya nchi miti itasaidia upatikanahi wa mvua kupunguza ongezeko la joto la hewa ukaa kwa sababu miti hudhalisha hewa ya okisjen na kusaidia ikolojia.
Mwanafunzi wa shule ya Doto Biteko sekondari Sarah Vedasto akipanda mti kwaniaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Bukombe Litengano Mwalwiba baada ya kuteuliwa na Mkurugenzi apande na kuutunza kwa niamba yake.
Sarah ameshukuru sana kwa kuteuliwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri nakuwa na tarajia kupanda not wa kiongozi mkubwa hivyo no ishara nzuri katika ndoto zake.
Mwalwiba akitoa shukrani kwa wananchi kuhudhulia kupanda miti amewaomba kuendelea kutunza mazingira na uoto wa asili.
Ofisa Tawala Wilaya Aly Mketo akizungumza kwa niamba ya Mkuu wa wilaya amewataka TFS kufanyakazi wito wa mwenyekiti na kwamba walimu na wanafunzi wahakikishe miti iliyo pandwa shuleni hapo ili kutunza mazingira.
MWISHO
Comments
Post a Comment