MKAZI WA GEITA AFARIKI DUNIA KWA KUSOMBWA NA MAJI

 

Mtu mmoja alietambulika kwa jina la Benjamin John (30) mkazi wa Mtaa wa Nyampa kata ya kasamwa halmashauri ya mji wa Geita, mkoani Geita amefariki dunia kwa kusombwa na maji katika mto Nyampa uliopo Mtaa wa Nyampa kata ya kasamwa Mkoani humo wakati alipokuwa ananawa miguu baada ya kumaliza kulima.


Kaimu Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Geita INSP. Edward Lukuba amesema Mtu huyo amefariki dunia kutokana na ajari ya mafuliko baada ya kumaliza shughuli zake za kilimo kisha kwenda kuoga kwenye mto huo hali iliyosababisha kusombwa na maji.


Mganga mfawidhi wa kituo cha afya kasamwa Emmanueli Alex amethibitisha kutokea kwa kifo hicho amesema mwili wa marehemu ulifikishwa katika kituo hicho na asikari wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Geita na walipoufanyia uchunguzi walibaini amekufa kwa maji na haukuwa na jeraha lolote.


Wananchi wa mtaa wa Nyampa kata ya Kasamwa halmashauri ya mji Geita wameiomba serikali kuwajengea kivuko katika mto huo kutokana na kuwepo na matukio ya mara kwa mara ya watu kuuwawa kwa kusombwa na maji wakivuka kwenda kwenye shughuli zao za kilimo.

Comments