AFARIKI KWA KUNYWA SUMU KISA KUHOFIA KUDAIWA 47,000

 

Kijana mmoja alietambulika kwa jina la Bukindu Mhoja (22) Mkazi wa Kijiji cha Bukoli kata ya Bukoli halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita amefariki dunia baada ya kunywa sumu akihofia kudaiwa elfu 47000.



Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi Ally Kitumbu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema kijana huyo amefariki kwa kunywa sumu huku Jeshi hilo likiendelea na uchunguzi Zaidi wa tukio hilo.


Baadhi ya ndugu zake na marehemu akiwemo mama yake wamesema kijana huyo aliagizwa dukani kwenda kununua soda alipofika dukani akatoa pesa ili ahaudumiwe lakini alipotaka kubeba soda hizo mwenye duka alimwambia bado hajalipa hali iliyosababisha kiajana huyo kurudi nyumbani na kuchukua maamuzi ya Kunywa sumu ndipo walipompeleka hospitalini hali iliyopelekea umauti wake.

Comments