TRA GEITA YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUTUNZA KUMBUKUMBU

 

.


Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Mkoa wa Geita imewataka Wafanyabiashara Wilayani Bukombe Mkoani Geita kutunza kumbukumbu za biashara zao ikiwa ni suala la risiti za manunuzi, mauzo na gharama za biashara Ili kuwawezesha kulipa kodi stahiki kwa mujibu wa sheria. 


Hayo yamebainishwa na Afisa Elimu na huduma kwa Mlipa kodi Jastine Katiti wakati wa semina iliyotolewa na TRA Mkoa wa Geita kwa wafanyabiashara Wilayani Bukombe ili kuwajengea uwezo wa namna bora ya kutunza kumbukumbu za biashara zao. 


Katiti amesema kuwa wafanyabiashara wamekuwa na mwitikio mdogo wa kutoa risiti wakati wa kuuza bidhaa zao pamoja na manunuzi mbalimbali wanayaoyafanya kwenye biashara zao hawadai risiti hali inayosababisha serikali kukosa mapato. 


Amesema adhabu za kukwepa kutoa risiti ni kali ambayo Kwa mujibu wa sheria ni kuanzia Milioni 3 hadi Milioni 4.5 aidha mnunuzi asipodai risiti adhabu yake ni kati ya elfu 30 hadi Milioni 1.5.


 Wafanyabiashara hao wameipongeza TRA Mkoa wa Geita kwa kuandaa semina hiyo na kuwapa elimu ya umuhimu wa kutunza kumbukumbu na kulipa kodi Kwa mujibu wa sheria na kuomba semina ziwe zinafanyika mara kwa mara .

Comments