MZEE ANAOZESHA WAKE ZAKE KWA WANAUME YOYOTE ATAKAEMPENDA.

 


Mzee mmoja anaejulikana kwa jina la Lusanika Malunguja Mkazi wa Kijiji Cha Nyamgogwa wilaya ya Nyan’ghwale Mkoani Geita amewashangaza watu wengi kwa kitendo chake cha kuwaozesha wake zake pindi mwanaume anapomtaka mke wake.


Mzee huyo amesema mwanaume yoyote akimpenda mke wake na wakakubaliana kuoana yeye hana shida kikubwa nikwenda kwake kujitambulisha na kumtolea Mahali kisha anamchukua.


Amesema sababu za kufanya hivyo ni kutokana na kila akioa mwanamke mzuri wanaume wanampenda kutokana na yeye kuwa masikini hali inayosababishwa nay eye kuishi na watu 100 katika familia yake. Mzee huyo ambae anajishughulisha na shughuli za kilimo amesema katika familia yake anaishi na watu mia moja wakiwemo watoto wake pamoja na ndugu zake.


Mzee huyo amesema Mpaka sasa ameshaozesha wake zake wawili baada ya wanaume waliochukua wake zake na baadae kuja nyumbani kujitambulisha na kutoa mahali kwa mzee huyo.

Amesema hata sasa mwanaume yoyote anaetaka kuoa mke wake anamruhusu kikubwa anachotaka mwanaume huyo aelewane na mke wake wakikubaliana yeye hana tatizo kuwaozesha baada ya kutoa mahali.


“Hayo maswala yalinitokea kwa sababu nilikua masikini sana nilikua sina chochote watu wananicheka nikileta mwanamke mzuri wanampenda kwa sababu nipo masikini umasikini ulukuja kwa sababu ya kuishi na watu mia moja watu wakawa wanawapenda wake zangu. 


“watoto nawashukuru sana kwa sababu walichukua mke wangu wakaja kujisalimisha na ukali ukatoka na mimi sio mkali walipokuja wakanipa ng’ombe tatu mara ya pili mwingine wakaja tena wakatoa mahali kwa mke wa pili, hata sasa akija mwingine asiniulize mimiaende kwa mke wangu akamuulize mwanamke akikibali mahali watapanga wenyewe mahali wataniletea” Amesema Mzee Lusanika.

Comments