WACHIMBAJI WADOGO WATAKIWA KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA.

 


Wachimbaji wadogo wa madini mkoani Geita wametakiwa kujiunga na Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kujilinda pamoja na kupata huduma ya matibabu ya uhakika wakati wa changamoto mbalimbali katika shughuliza uchimbaji wa Madini.


Rai hiyo imetolewa na Meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa Geita Bw. Elias Odhiambo katika maonesho ya tano ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili Mkoani Geita.



Bw. Odhiambo amesema achimbaji wa madini wanatakiwa kuwa na bima ya afya kwa lengo la kuwalinda na pindi wanapopata changamoto yoyote ya kiafya wanakuwa na uhakika wakupata matibabu kwa wakati.


Amesema wametumia nafasi ya uwepo wa maonesho haya ya kitaifa ya  teknolojia ya madini kuwafikia wachimbaji wadogo katika mabanda yao ili kuwahamasisha wajiunge na mfuko wa taifa wa bima ya taifa.


Amesema mwitikio kwa wachaimbaji wadogo wa madini mkoani Geita pamoja na watu mbalimbali katika  kujiunga na bima ya afya ni Mkubwa kutokana na kuwapa elimu ya kutosh juu ya umuhimu wakuwa na bima ya afya.


Nao baadhi ya washiriki katika maonesho hayo waliotembelea banda la NHIF akiwemo Bw. Renatusi Kduduha amekiri kuwa bima ya afya ina umhumu Mkubwa katika kusaidia wakati wa matibabu pale uanpougua ama kuuguliwa kutokana na gharama za matibabu kupanda hivyo ukiwa na bima unapata huduma kwa urahisi zaidi.

Comments