RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI KWA MARA YA KWANZA MKAONI GEITA.

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kikazi mkoani Geita Kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kuwa rais wa Tanzania.


Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amesema Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kikazi mkoani Geita Kwa siku mbili kuanzia  October 15 & 16, 2022.


Katika ziara hiyo Mhe, Rais atatembele hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Chato na kupokea taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo kwa lengo la kujonea jinsi hospitali hiyo inavyotoa huduma za kibingwa, pamoja kituo cha kupozea umeme Mpomvu na kukifungua.


Shigela amesema Mhe Rais Samia atapokelewa wilayani Chato akitokea mkoani Kagera amewataka wananchi wa wilaya ya Chato na viongozi mbalimbali wa mkoa kujitokeza kuanzia 12:00 asubuhi kumpokea Mhe. Rais pindi atakapo wasili wilayani chato Mkoani Geita.


"Naomba kutoa wito kwa wananchi wote wa mkoa wa Geita pamoja na viongozi mbalimbali ngazi ya mkoa, viongozi wa dini, wazee na wale wa Chama cha Mapinduzi tujiandae kumpokea Mgeni wetu, ambapo ni mara ya kwanza kufanya ziara ya kikazi mkoani Geita tangu alipo apishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Amesema Shigela.

 

Aidha  Shigela amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kuhakikisha hadi ifikapo leo October 13, 2022 majira ya saa 9:00  alasiri,vitabu vyote vya kupokelea wageni katika nyumba za kulala wageni (Guest Houses) vilivyo chukuliwa  viwe vimerudishwa vyote kwa wahusika.

Comments