DAWA MBANDIA ZA NGUVU ZA KIUME ZADAKWA GEITA.




Mamalaka ya dawa na vifaa tiba kanda ya ziwa magharibi (TMDA) imekamata dawa bandia  za kuongeza nguvu za kiume zinazotumiwa na vijana kwa lengo la kuongeza nguvu za kiume  wakati wa tendo la ndoa.



Meneja wa Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) kanda ya ziwa magharibi Dkt. Edgar Mahundi amesema mamlaka hiyo imekamata dawa bandia zinazotumika kwa matumizi ya kuongeza nguvu zilizokuwa zinauzwa katika maduka ya madawa kinyume na sheria.


Dawa hizo zizazotambulika kwa jina la Vega 100 zimekuwa zikitumiwa kiholela  na kwa wingi  na vijana wa kiume kwa lengo la kuongeza kuvu za kiume wakati wa tendo la ndoa.


Amesema dawa hizo ni bandia na hazijathibitishwa na Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA)  amewataka vijana kuachana na matumizi ya dawa hizo kwani zina athali kubwa kiafya na hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Comments