SHIGELLA AWASILI GEITA ASISITIZA KUWATUMIKIA WANANCHI.



Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe, Martin Shigella amewataka viongozi mbalimbali mkoani Geita  kushirikiana kwa pamoja kwa lengo la kuwatumikia wananchi hali itakayochochea kukua kwa maendeleo ya mkoa huo.


Mhe Shigella amesema hayo leo 5.8.2022   alipowasili Mkoani Geita  na kupokelewa na viongozi mbalimbali katika ofisi ya Mkuu wa moa iliyopo Magogo mkoani Geita.


Amewataka viongozi mbalimbali kushirikiana katika nutendaji kazi ili kutimiza adhima ya serikali yakuwahudumia wananchi amesema atahakikisha anasimamia vyema katika ukusanyaji wa mapato katika halmashauri za mkoa wa Geita ili kufikia malengo ya mkoa.


Amesema viongozi wanapaswa kuwafata wananchi katika maeneo yao ili kuktatua kero zao na kuachana na kasumba ya kukaa ofisini ili wananchi wawafate katika ofisi zao kwa lengo la kutatuliwa kero zinazo wakabili kwani wamechaguliwa katika nafasi zao mbalimbali kwa lengo la kuwatumikia wanchi.


Mhe Shigella kabla ya kuteuliwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassani kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

 

 “nafarijika kuja kufanya kazi nanyi wanageita kwakua Mkoa wetu una agenda mkoa wetu una watu wanaojituma kutafuta maendeleo kwa bidii nami na viongozi wenzangu tutashirikiana nayi kuhakikisha maendeleo yanapatikana kikubwa niendelee kusisitiza

 mshikamano,upendo na ushirikiano hiyo ndio iwe nguzo yetu itakayotuvusha” amesemaMhe, Martin Shigella.


Awali Kaimu katibu tawala wa Mkoa wa Geita Herman Matemu alipokuwa akiwakilisha taarifa mbele ya Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe, Martin Shigella amesema Mkoa wa Geita ni salama kutokana na kudhibiti matukio ya uhalifu kuanzia ngazi ya mitaa hivyo kuufanya Mkoa kuendelea kuwa salama.


 “Miradi balimbali ipo katika hatua zinazoridhisha ikiwemo ujenzi wa uwanja wa mpira,ujenzi wa nyumba ya makazi ya Mkuu wa Mkoa ujenzi wa ofisi na nyumba za makazi za wakuu wa Wilaya Mbongwe na Nyang’hwale”amesema Matemu.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Saidi Mkumba kwa niaba ya Wakuu wa wilaya ya Geita amesema wakuu wa Wilaya za Geita kwa pamoja wanaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuchochea maendeleo ya mkoa wa Geita.


Amesema wanamfahamu Mhe Shigella kwa utendaji kazi  hivyo wao  wako tayari kufanya kazi  kwa bidii ili kutimiza vyema adhima ya kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa kuwatumikia wananchi.


 “sisi kama wasaidizi wako tunakuahidi kuwa tutafanya kazi ya kuleta maendeleo kazi ya kutatua kero za wananchi na tunaamini sasa tunaenda kujenga misingi imara ya utendaji kazi na itakua kazi ya muendelezo aliyoiacha mama yetu Rosemary Senyamule aliyokua akiifanya kwa kushirikiana nasi” amesema Mkumba

Comments