WATU 3 MBARONI TUHUMA ZA KUUA MAMA YAO MZAZI WAKITAKA SHAMBA LA URITHI.

Watu watatu wanashikilia na Jeshi la Polisi Mkoni Geita kwa tuhuma za mauaji ya mama yao  mzazi alietmbulika kwa jina la Milembe Lutubija (70) mkazi wa Kijiji cha Nyaruyeye, Kata ya Nyaruyeye ,Tarafa ya Busanda Wilaya ya Geita.


Kamanda wa  Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi Henry Mwaibambe  amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema limetokea Juni 1,2022 Majira ya Saa Moja Jioni.


Mwaibambe  amesema chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa kifamilia ambapo watoto hao walikua wanataka kupewa urithi wa mashamba na mama yao.


Amesema kuwa watoto  hao ni  Jumbe Kifoda(36),Dotto Kifoda(34) na Lukina Kifoda(30) walishirikiana na kumuua mama yao kwa kumkata na kitu chenye  ncha kali kichwani na mikono ya kulia na kushoto na mpaka kusababisha kifo chake.


Mwaibambe amesema Mama yao aliwataka watoto wake waondoke nyumbani ili waende kujitegemea lakini watoto hao wakawa hawataki na kuanza kushinikiza kugawiwa ardhi ya shamba ambalo lilikuwa ni mali ya Mama yao.


Kamanda Mwaibambe amesema kuwa mwenendo wa watuhumiwa hao ukionyesha kuwa wali Kuwait wanaahidi mara kwa mara kumuua mama yao kwasababu ya kuwafukuza kwenye shamba hilo.


Hata hivyo Kamanda Mwaibambe amesema watuhumiwa wote wamekamatwa na baada ya Upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani.

Comments