RAISI SAMIA AWATAKA WAKAZI WA CHATO KUVUTA SUBIRA JUU YA ARDHI YA HIFADHI YA CHATO


 Serikali imewataka wakazi wa kata Bwanga wilayani Chato Mkoani Geita kuwa na subira juu ya ulekebishaji wa mipaka ya hifadhi  ili kuwapa fursa ya kutumia eneo hilo katika shughu  mbalimbali za kibinadamu.


Akizungumza na wananchi wa kata ya Bwanga iliyopo wilayani chato mkoani Geita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan amewataka wakazi hao kuwa na subira juu ya ulekebishwaji wa mipaka ya hifadhi ili kuruhusu kuanza kutumika katika shughuli za kibinadamu.


Raisa Samia amesema tatizo la uhaba wa ardhi sio Bwanga tu bali ni nchi nzima kutokana na mahitaji ya aridhi kuwa makubwa  hivyo amawetaka wakazi hao kuwa watulivu  hadi pale serikali itakapo toa ruhusa juu ya matuzi ya ardhi ya hifadhi katika shughuli za kibinadamu.


‘’Tutachukua hatua ya kuangalia hifadhi zetu na mipaka yake halafu tutatoa maamuzi” amesema Rais Samia Suluhu Hassan.


Wananchi hao walikua wanaomba kwa mhe, Rais kupewa ruhusa ya kupata ardhi  kutoka katika hifadhi ya shamba la miti la Silayo ili waweze kuzitumia katika shughuli za kibinadamu.


Awali Mbunge wa Jimbo la Chato Mhe, Medard Kalemani wakati akizungumza na wananchi hao mbele ya Rais Samia  Kalemani alimuomba Mhe, Rais kuridhia ombi la wananchi hao la kutoa kilomita 8 kutoka katika sehemu ya ardhi ya shamba miti la silayo.


Nae mkuu wa mkoa wa Geita Mhe, Rosemary Senyamule amempongeza Mhe, Rais kwa kutoa fedha zaidi ya bilioni 190 kwa lengo la kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya mkoa wa Geita.

Comments