WAFANYABIASHARA 8 WA MADINI WAKAMATWA TUHUMA UTOROSHAJI DHAHABU-GEITA.

Wafanya biashara wa Madini ya dhahabu wapatao nane wamekamatwa  mkoani Geita  kwa tuhuma za utoroshaji wa madini.


Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Dkt. Doto  Biteko wakati wa ziara yake katika Kata ya Rwamgasa Wilaya ya Geita mkoani Geita ambapo amesema Wizara hiyo imefanya msako baada ya kubaini dhahabu inayozalishwa kwa kutumia kemikali ya zebaki imepungua sokoni.


Amesema kuwa wafanya biashara hao wamekamatwa  kufuatia  msako unaendelea baada ya Wizara yake kubaini mauzo ya Dhahabu inayotokana Zebaki kushuka katika masoko hapa nchini hivi karibuni.


Dkt. Biteko ametumia nafasi hiyo kuwataka wafanyabiashara kutojihusisha na utoroshaji wa Madini kwani watakamatwa na kuchukuliwa hatua Kali Kwa mujibu wa Sheria za nchi.

Waziri Biteko amewatahadhalisha wanunuzi wa Madini kote nchini kuendelea kuuza Dhahabu kwenye masoko  halali na kuacha kununua Madini mitaani ili kuepuka mkono wa Sheria.


Aidha Dkt.  Biteko amepiga marufuku wachimbaji wadogo wa dhahabu nchini kuacha mara moja tabia ya kujenga mialo ya kuchenjua Dhahabu majumbani kwao wanapoishi badala yake yatengwe  maeneo maalum kwa ajili ya shughuli hiyo.






Comments