RAIS SAMIA AMKABIDHI TUZO MSANII WA HIP HOP JOSEPH MBILINYI "SUGU"


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimpa Tuzo Msanii wa Muziki wa Hiphop nchini Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ya kuthamini mchango wake katika Sanaa na kuzalisha ajira kabla ya kuzindua kitabu cha msanii huyo chenye jina la Muziki na Maisha from the Street katika Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kitabu cha Msanii Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ chenye jina la Muziki na Maisha from the Street katika Tamasha la Dream Concert lililofanyika Serena Jijini Dar es Salaam.






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na msanii wa Muziki wa Hiphop Bw. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ mara baada ya kuwasili Serena kwa ajili ya kuhudhuria tamasha la maadhimisho ya miaka 30 ya msanii huyo.

Comments