SERIKALI KUENDELEA KUHAMASISHA WAWEKEZAJI SEKTA YA MADINI

 

Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Dotto Biteko amesema Serikali imeendelea kuhamasisha wawekezaji kuwekeza katika Sekta ya Madini ili kuongeza mchango wa sekta katika Pato la Taifa. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Wizara kupitia Tume ya Madini imetoa leseni mbili (2) za uchimbaji mkubwa wa madini ya dhahabu kwa kampuni ya Sotta Mining Corporation Limited inayomilikiwa na Nyanzaga Mining Company Limited na Serikali na leseni ya madini ya nikeli kwa kampuni

Ameyasema hayo leo Bungeni wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
“Serikali imekamilisha mazungumzo na kampuni ya uchimbaji wa madini ya almasi ya Williamson Diamond Limited ambapo hisa za Serikali zimeongezeka kutoka asilimia 25 hadi asilimia 37.”

Aidha,Amesema Serikali imesaini mikataba na kampuni za uchimbaji wa madini ya graphite kwa kampuni ya Mahenge Resources Limited (Black Rock Mining Ltd) na madini ya heavy mineral sands Kampuni ya Jacana Resources Limited (Strandline Resources Ltd) na kuunda Kampuni za ubia za Faru Graphite Corporation na Nyati Mineral Sands Ltd mtawalia. Serikali ni mbia katika kila kampuni kwa kumiliki hisa asilimia 16 zisizoshuka thamani.

Comments