WANANCHI WA AHIDI KUMUUNGA MKONO MBUNGE


Wananchi wa Kata ya Ng'anzo Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita wamempongeza  Mbunge wa Jmbo la Bukombe Dkt Doto Mashaka Biteko kwa kukamirisha vyumba viwili vya madarasa hali ambayo imewafanya wanafunzi wa Kidato cha kwanza mwaka 2022 kuanza kusomea kwenye madarasa na kuondokana na changamoto ya kutembea umbari mrefu kuafuata huduma ya Elimu.

Mkazi wa Ng'anzo Joseph Malale akitoa pongezi hizo alisema Mbunge alitoa Tsh milioni 2.5  kwa ajili ya mabati.

Malale alisema katika Ujenzi unaoendela kwa sasa vijana wamepata ajira ya Ufundi na pamoja na vibarua vya vidogo vidogo.



Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Ng'anzo Asia Njalikai akiungana na wananchi kumpongeza Mbunge Dk Biteko alisema nguvu za wananchi katika mradi huo ni  Tsh 8,288,000 huku halmashauri imetoa bati 240 zenye thamani ya sh 6,840,000.

 Njalikai alisema jitihada za Mbunge zimepelekea serikali  kuleta Tsh milioni 470 kwa ajili ya madarasa manane maabara tatu makitaba moja jengo la utawala moja chumba cha tehama kimoja pamoja na matundu 20 ya vyoo.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Mbunge pamoja na madiwani wanapo hamasisha ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwa lengo la serikali nikusogeza huduma kwa wananchi



Comments