“Tumeona thamani ya fedha kwenye miradi ya DAWASA” PAC

 

Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na thamani ya fedha katika utekelezaji wa miradi ya majisafi katika Jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani.

Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara ya kamati katika mradi wa maji Makongo hadi Bagamoyo uliogharimu kiasi Cha sh. Bilioni 65 na kuonyesha kuridhishwa na utekelezaji wa wake.

Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge hesabu za Serikali Mh. Japhet Hasunga (Mb) ameeleza lengo la ziara hiyo ililenga kukagua thamani ya fedha zilizotolewa na kutekeleza katika miradi mbalimbali inayosimamiwa na DAWASA.

“Sisi kama kamati ya Bunge tumefanya ziara hii Ili kuona na kutathmini thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali katika mradi mbalimbali, na kwa niaba ya Kamati nikiri kuwa tumeridhishwa sana na kazi zilizotekelezwa na DAWASA na kila mmoja wetu amejionea na kuridhika na kiasi cha fedha kilichotumika kwenye miradi hii.”ameeleza Mh.Hasunga

Aidha Mh.Hasunga ameongeza kuwa pia lengo la ziara ilikuwa kuona namna bodi ya wakurugenzi DAWASA inavyowajibika katika kusimamia miradi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya Serikali.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange ameieleza kamati kuwa mojawapo ya siri yakufanikiwa katika utekelezaji wa miradi ya maji ni kutokana na uongozi mzuri uliopo na weledi mkubwa baina ya Menejimenti na watumishi.

“Tumepata mafanikio hasa katika kusimamia miradi mbalimbali ikiwemo huu wa kuanzia Makongo hadi Bagamoyo kutokana na kufuata sheria na taratibu zilizopo zinazoongoza Mamlaka na mashirika ya Umma”.ameleeza Jenerali mstaafu Mwamunyange

“Tunafurahi kuona Kamati imeridhika na kazi kubwa tunaiyofanya ya usimamizi wa fedha na utekelezaji wa miradi kwa thamani halisi ya hela, hii inatutia moyo sana na tunawaahidi uwajibikaji zaidi ili kufikia malengo yaliyowekwa” ameongeza Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange.

Mradi wa maji *Makongo hadi Bagamoyo* unatekelezwa kupitia fedha za wadau wa maendeleo na kusimamiwa na DAWASA kwa gharama ya kiasi cha Tsh Bilioni 64. Mradi utakapokamilika utahudumiwa wakazi zaidi ya 450,000 wa maeneo ya Changanyikeni,Vikawe, Goba, Bunju, Madale,
Wazo, Ocean Bay, Salasala na sehemu ya mji wa Bagamoyo

Comments