HITIMISHO LA KAMBI YA MAZOEZI TIMU YA BUKOMBE COMBINE SPORTS CLUB

 

Wachezaji wa Timu ya Bukombe Combine Sports Club iliyopo Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wameupongeza uongozi wa timu hiyo kwa kuwatambua na kuwapa vitamburisho vya CLUB.

Shukrani hizo zimetolewa na wachezaji wa timu hiyo kwa nyakati tofauti baada ya kambi ya mazoezi kuhitimishwa na kuchaguliwa kuwa miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo.

Mchezaji Oswardi Venace amesema kitabulisho alicho pewa kimemfanya kuwa na furaha na kujiona kama amepanda daraja hata akiitwa sehemu nje na timu yake kitamburisho kimemuongezea hadhi.

Katibu Msaidizi wa Bukombe Combine Sports Club Jonathan Mgaya amesema vitamburisho hivyo vitawatambulisha kokote watakapo enda kucheza na uongozi kuwasapoti popote pale mchezaji atakapo omba msada ili kuhakikisha usalama wa mchezaji wakati wote.

Mwenyekiti wa CLUB hiyo Nelvin Ndugu amesema wachezaji walikuwa 120 na waliobaki baada ya kambi ya mazoezi kumalizika ni wachezaji wa mpira wa miguu  30.

Ndugu amewaomba wachezaji hao watakapo kuwa nyumbani waendelee kufanya mazoezi mbalimbali ili watakapo  kwenda kukutana na timu nyingine kujipima kuonyesha Bukombe kuna mpira.

Mwenyekiti alimshukuru Kocha Mkuu Mengire Hobbu na kocha msaidizi James Kishimba  kwa kukaa na wachezaji siku tatu kambini kwa lengo la kupata wachezaji bora.
 





Comments