WANACCM BUKOMBE WAHAMASISHWA KUJITOKEZA KUGOMBEA

Wananchama wa Chama Cha Mapiduzi CCM Wilaya ya Bukombe Mkoani 
 Geita wametakiwa kujitokeza  kugombea nafasi za uongozi mbali mbali ndani ya Chama kwenye Uchaguzi utakao fanyika kuanzia ngazi ya matawi mwaka huu.

Wito huo umetolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Bukombe Odilia Bathromayo kwenye madhimisho ya sherehe za miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM Wilaya ya Bukombe yaliyofanyika katika Uwanja wa mwenge Kata ya Uyovu.

Bathromayo alisema ratiba ya uchaguzi ndani ya chama imetoka na itapelekwa kwenye ngazi ya kata hadi matawi ili kila mwanachama aweze kugombea uongozi kwenye chama. 

"Kauli mbiu ya Uchaguzi huu ni Shiriki Uchaguzi kwa UadMacho"Alisema Katibu Odiliango

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe Daniel Machongo alisema wakati ukifika wanachama wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi mbali mbali ili kukiletea maendeleo ya chama.

Alisema CCM kufikisha miaka 45 kitaendelea kuishauri serikali yake ili iendele kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa kuwasogezea huduma wananchi.

Nae Diwani wa Kata ya Uyovu Inyasi Kulusanga  alisema tangu achaguliwa Udiwani amesimamia miradi ya maendeleo kwa kushirikiana na wananchi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dk Doto Biteko wamejenga vyumba tisa vya madarasa na Kituo cha Afya kupanda hadhi na kuwa Hospitali kwa muda wa Mwaka mmoja.













 

Comments