Shule za Sekondari kumwagiwa Fedha za Ujenzi wa Maabara-Bukombe

 

Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita imepokea Tsh milioni 150 kwa ajili ya ukamilishaji  wa maabara ili wanafunzi waanze kujifunza kwa vitendo hasa masomo ya sayansi.

Amebainisha Mkuu wa Wilaya YA Bukombe Said Nkumba wakati akitowa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM 2020 hadi 2025 katika mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe.

Nkumba alisema serikali katika kutekeleza Ilani ya CCM mwezi Julai hadi Desemba 2021 halmashauri imepokea Tsh bilioni 2.1 fedha kutokana mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mpango wa mapambano ya Uviko 19.

Alisema kati ya fedha hizo zimejenga vyumba vya madaraza 107 madarasa 43 shule ya msingi shikizi na 64 shule za sekondari 17 wilaya hapa.

 Aidha serikali imeleta Tsh milioni 112.5 katika shule tano za sekondari kwa ajili ya ukamirishaji wa vyumba vya madarasa ikiwemo Tsh milioni 470 kwa ajili ya ujezi wa shule mpya ya Nganzo Sekondari ambapo taratibu za kuzihamisha fedha hizo kwenda kwenye akaunti za vituo vya kutolea huduma zinaendelea.

MWISHO

Comments