MWENYEKITI WA CCM MKOA WA GEITA APONGEZA UTEKELEZAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOMBE BAADA YA MAAGIZO YALIYOTOLEWA NA WAJUMBE KAMATI WA SIASA MKOA
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita Said Kalidushi amewataka watalamu wa Halmashauri kuendelea kushirikiana vizuri na viongozi wa chini kusimamia fedha za serikali kuu na mapato ya ndani ili miradi iendelee kukamilika kwa wakati.
Kalidushi alitoa wito huo Januari 14,2022 wakati akipongeza utekelezaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe baada ya maagizo aliyoyatoa 2021 wakati wa ziara yake na Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa katika ziara hiyo alitoa maelekezo ya huduma za kuchinja mifungo katika machijio ya Mifungo Kijiji Cha Mwalo isitishwe hadi watakapo fanya ukarabati kutokana na kuwa na mazingira yasioridhisha.
Kalidushi alisema kwa jitihada ambazo Wataalanu wa Halmashauri na Viongozi wa serikali ya Wilaya waliyoionyesha kwa kutekeleza kwa kuanza ukarabati wa machinjio ya mifungo yaliyopo Kitongoji cha Bwenda Kata ya Katente kwa thamani ya sh 10.5 milioni hali ambayo itaboresha vizuri huduma za wananchi.
Awali Afisa Mifugo Msaidizi Wilaya ya Bukombe Rashid Omary alisema Halmashauri katika kutekeleza maelekezo ya Kamati ya Siasa Mkoa wametumia Tsh milioni 10.5 ambayo ni mapato ya ndani na kati ya fedha hizo TSh milioni 8.7 zimetumika kukarabati miundombinu ya machinjio na Tsh milioni 1.8 zimetumika kwa ajili ya kununua mashine ya maji kwenye eneo hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukombe Yusuph Mohamed alisema walitekeleza maagizo ya kuhamisha machinjio ya Mwalo kwa kupisha ukarabati na kuhamishia huduma katika machinjio ya Bwenda Katente.
Mohamed alisema katika utekelezaji wa maelekezo ya Kamati ya Siasa Mkoa juu ya ukarabati wa machinjio ya Mwalo tayali wamesha pokea boksi 150 za vigae na Vyuma kwa ajili ya kuning'iniza nyama katika machinjio na Halmashauri inatarajia kuendelea na ukarabati ili huduma zilejee katika machinjio makubwa ya Mwalo.
Comments
Post a Comment