Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoa wa Geita. Yusuph Mohamed amewaomba madiwani kushirikiana nawatalamu wanapo kuwa na mikakati ya kusogeza huduma kwa wananchi.


Hayo ameyaeleza leo Novemba 25, 2021 kwenye baraza la madiwani baada ya diwani wa kata ya Ng'anzo Mashaka Shinwenda kuomba huduma ya mama na mtoto watalamu wa afya watumie ofisi ya kata wakati ujenzi wa Zahanati ukiendelea.


Shinwenda amesema kata hiyo haina Zahanati wala kituo cha Afya na huduma ya inayotolewa na watalamu wa Afya wanatowa kwenye mikoba kwenda na kurudi huku huduma zingine za mama na mtoto hurazimika kufata Ushirombo hospitali ya wilaya.


Mohamed amesema baraza la madiwani limeazimia mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kushirikiana na mganga mkuu wa wilaya Dk Olden Ngasa kuona umuhimu wa kutengeneza mazingira mazuri ili huduma ya mama na mtoto ianze kutolewa bira kuathiri kanuni na sera za afya.


Awali diwani wa Bulenga Erick Kagoma wakati akichagia hoja hiyo aliomba diwani wa kata hiyo kuhamasisha ujenzi wa miundombinu Afya ikiwa huduma za kiliniki ya mama na mtoto haitakiwi kutolewa Sehemu isiyo sahihi.


Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Bukombe Lutengano Mwalwiba alikata maombi hayo nakuongeza kuwa anafanyakazi kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu na miongozi ya kiutumishi kanuni haziruhusu huduma ya mama na mtoto kutolewa ofisi ya kata au sehemu ambayo siyo sahihi.


Amesema badalayake diwani anatakiwa hamasishea wananchi ili wakamirishe Zahanati na kituo cha Afya.


Mwalwiba amesema wananchi wa Ng'anzo huduma za afya wananchi wanafata mbali huku huduma za afya zinazo tolewa kwa mkoba kiliniki ya mama na mtoto  zinatilewa mara tatu tofauti na kata zingine ambazo huduma hizo hutolewa mara mbili kwa wiki.


MWISHO

Comments