Rc Geita awataka Mawakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Kutunza Vyanzo vya Maji





  Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule  ameagiza Mawakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijiji Mkoani humo kufanya mazungumzo na wananchi ambao wanafanya shughuli za kilimo kwenye maeneo yanayozunguka vyanzo vya maji  wapishe ili  kuvinusuru vyanzo hivyo pamoja na kupanda miti rafiki na maji ili kutunza Mazingira.

Senyamule ametoa agizo hilo leo Desemba 29, 2021 wakati akikaguwa chanzo cha maji kilichoko Kitongoji Cha Gengeni Kijiji cha Nampalahala Kata ya Busonzo Wilayani Bukombe na kukuta mazingia karibu na chanzo hicho cha maji wananchi wamelima mazao.

 "Hakiksheni munazungumza nao na wanasitisha shughuli za binadamu kwenye vyanzo vya maji ili maji baadae yasije yakakauka kwa kushindwa kutunza mazingira.amesema Rc Senyamule.

Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Yusuph Mohamed amesema wanalipokea na atalifanyia kazi ili wananchi walipwe fidia na wapishe kwenye vyanzo vya maji.

Awali Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA Wilaya ya Bukombe James Benny amesema ameshazungumza na Afisa Mazingira wa Wilaya ya Bukombe ili kupata miti na kuanzia Januari anatalajia kuanza kupanda miti kwenye vyanzo vyote vya maji.

Benny amesema mradi wa maji  katika Kijiji cha Nampalahala Kata ya Busonzo ulianza Februari 2019 unatarajia kukamirika Januari 2022 hadi kukamilika utaghalimu Tsh Bilioni 1.1  na itahudumia wakazi 6108 katika Kijiji cha Nampalahala.

Amesema fedha hizo amejenga miundombinu mbalimbali ikiwemo Nyumba ya Mlinzi,Tenki dogo lenye ujazo wa lita 50, 000 na Tenki kubwa lenye ujazo wa lita 225,000 pamoja na ofisi za watoa  huduma na vituo nane vya kuchotea maji.

Amesema chanzo kikubwa cha maji katika mradi huo ni kisima kirefu kilichopo kitongoji cha Gengeni ikiwa ujenzi  wa mitandao ya kusambaza na kutoa huduma kilomita 21.1 na fedha iliyo tegwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu ni sh 1.1 bilioni  fedha iloyolipwa sh889.7 milioni.

Kwa Upande wake Mkazi wa Kijiji cha Nampalahala Mather Wilison amesema kabla ya mradi huo wa maji kukamilika walikuwa wanaamka  usiku sana kufuata maji kwenye kijiji jirani cha Munekezi umbali wa kutembea masaa matatu kwenda na kurudi.

Comments