Uvccm watakiwa kujitolea Nguvu zao kwenye miradi ya Maendeleo.


 Mwenyekiti wa Umoja wa Jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Bukombe mkoani Geita Nelvin Salabaga amewataka vijana kujitolea nguvu zao kwenye ujenzi wa miradi ya maendeleo inayo fadhiliwa na wadau wa maendeleo,Wawakilishi,Serikali na wananchi kwa kuchimba misingi, kusogeza mchanga na mawe na maji ili  miradi ikamilike ikiwa  imebakiza fedha na kufanya maendeleo mengine.


Alitoa wito huo Oktoba 30 wakati akihitimisha ziara yake kwenye Kata 17 za Wilaya ya Bukombe baada ya kuona mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Namonge ambacho kimejengwa kwa nguvu za wananchi na serikali pamoja na nguvu za Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dk Doto Biteko.


Salabaga alianza ziara yake iliyoanza tarehe 20 Oktoba 2021 hadi Oktoba 29, 2021 ya kwenda anaagalia Uhai wa Jumuiya na kuimarisha UVCCM kuanzia ngazi ya tawi.



Katika maeneo mengine Mwenyekiti wa Jumuia ya vijana Wilaya aliona miradi ya ujenzi wa Zahanati Vituo vya Afya na miundombinu ya madarasa na vyoo shule za msingi na sekondari hali ambayo aliwapongeza wananchi kwa kuchangia nguvu zao na mali zao na Serikali kwa kuwaunga mkono wananchi.


Salabaga alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dk Biteko kwa kuwa mstali wa mbele kuhamasisha maendeleo kwa kuchangia fedha kwenye miradi mingi ya maendeleo hasa ujenzi wa miundombinu ya Shule na Afya.


Aliwaomba wananchi na viongozi wengine kuendelea kumuunga mkono Mbunge anapo hamasisha miradi ya maendeleo na kusimamia kikamilifu vitu vinavyo tolewa kwa ajili ya ujenzi ikiwa amekuwa akitoa Nondo, mifuko ya simenti, mabati na Tofali pamoja na fedha kwa ajili ya ukamirishaji wa miradi.








Comments