Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini kwenye Hafla ya Ufunguzi wa Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini iliyofanyika katika Viwanja vya Kituo cha Uwekezaji Cha EPZ Bombambili Mkoani Geita Septemba 22, 2021.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini kwenye Hafla ya Ufunguzi wa Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini iliyofanyika katika Viwanja vya Kituo cha Uwekezaji Cha EPZ Bombambili Mkoani Geita Septemba 22, 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule akizungumza na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini kwenye Hafla ya Ufunguzi wa Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini iliyofanyika katika Viwanja vya Kituo cha Uwekezaji Cha EPZ Bombambili Mkoani Geita Septemba 22, 2021.
Mgeni rasmi wa Maonesho Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau katika Hafla ya Ufunguzi wa Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini Mkoani Geita.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza Maonesho ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita kila mwaka kuwa ya kitaifa huku akitaka miundombinu katika maonesho hayo kubeba sura ya Kimataifa ili Geita itambulike kuwa Kitovu cha Dhahabu duniani.
Ametoa maagizo hayo, leo tarehe 22 Septemba 2021 wakati akifungua rasmi Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Kituo cha Uwekezaji cha Bombambili , Geita.
Akizungumza umuhimu wa maonesho Waziri Mkuu Majaliwa ameeleza, maonesho yamekuwa na manufaa makubwa katika kuhamasisha wananchi kujihusisha na shughuli za madini nchini ikiwemo kuwaweka karibu wachimbaji wadogo katika kutangaza fursa zilizopo katika Sekta ya Madini kwa manufaa ya Geita na Taifa.
"Manufaa hayo, tumeanza kuyashuhudia kwa migodi mingi kuanza kutumia huduma na bidhaa zinazozalishwa nchini kutoka kampuni za wazawa. Pia idadi ya Watanzania wanaoshiriki na kunufaika na uwepo wa rasilimali hizi imeongezeka," amesema Waziri Mkuu.
Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amesema, Sekta ya Madini imeendelea kutoa mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa na maendeleo ya mtu mmoja mmoja nchini. Amesema matarajio ya Serikali ni kuongeza zaidi mchango huo kupitia Shughuli za uchimbaji, uchenjuaji, usafishaji madini, usanifu madini na utoaji wa huduma katika shughuli za madini.
Akieleza changamoto za wachimbaji wadogo, amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri ya kusaidia wachimbaji wadogo kufikia malengo yao.
"Serikali imeweka mikakati ya kuimarisha Taasisi zake hususan Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na STAMICO ili taasisi hizo ziweze kutoa huduma bora na nafuu kwa wachimbaji wadogo," ameongeza Waziri Mkuu Majaliwa.
Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu Majaliwa ameagiza Wizara ya Madini kuhakikisha suala la Local Content linasimamiwa kikamilifu. Aidha amesisitiza kutumia CSR kama chachu ya kuleta maendeleo yenye tija kwa kizazi cha sasa na baadaye kwenye Halmashauri zote.
Naye, Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema, mafanikio yote yanayopatikana kwenye Sekta ya Madini, ni kwa sababu ya usimamizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Sukuhu Hasaan
"Mhe. Rasi Samia alitoa maelekezo mahususi kwa Wizara na Taasisi zake, ya kwanza nendeni kuwasikiliza wachimbaji wadogo, wa Kati na Wakubwa," ameeleza Dkt. Biteko.
Aidha, Dkt Biteko ameeleza kuwa, toka amepata maelekezo hayo mambo makubwa yamefanyika kwenye wizara na migodi mikubwa ambayo inaendesha shughuli za uchimbaj.
Akieleza kuhusu Sheria ya Local Content Dkt. Biteko ameeleza kuwa, Wizara imetoa maelekezo Maalum kuwa Local Content lazima itekelezwe. Amesema kazi kubwa ya kuchoronga inayokuja kwa Kampuni ya GGML ambayo inathamani ya Dola za Marekani Milioni 183 lazima Mgodi huo uungane na Kampuni za ndani.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule amesema Mkoa wa Geita unaongoza kwa uchimbaji na upatikanaji wa madini ya Dhahabu. Amesema kuwa zaidi ya asilimi 40 ya Dhahabu inayouzwa hapa nchini inapatikana katika mkoa wa Geita.
Maonesho ya Madini yaliyofunguliwa rasmi leo yalianza tarehe 16 Septemba yanatarajia kufungwa tarehe 26 Septemba 2021. Ufunguzi wa maonesho yamehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Wabunge na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini.
Comments
Post a Comment