
Afisa Mtendaji wa Kata ya Katente Issa Shabani akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye mkutano ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko.
Waziri wa Madini Doto Mashaka Biteko amewataka wachimbaji wadogo wadogo wa Madini ya Dhahabu waliokuwa wanachimba katika Mgodi wa Rushi iitwayo Namba Choo iliyopo Katente Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kufanya makubaliano na wakazi wanaouzunguka mgodi huo kwa Muhtasari baada ya maridhiano na kuyawasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
Biteko alisema Rushi hiyo ilifungwa na Serikali ya Wilaya kutokana na migogoro ya wakazi wa maeneo hayo na wachimbaji kwa madai ya wakazi wanaathilika na mgodi huo.
"Ili pafunguliwe na Serikali ya Wilaya lazima wahakikishe wachimbaji wamekaa na wakazi wa eneo linalozunguka mgodi huo na kwa vikao halali na nyaraka zifike Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na akijiridhisha atapafungua"Alisema Biteko.
Awali Afisa Mtendaji wa Kata ya Katente Issa Shabani wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na changamoto zinazo wakabili wachimbaji waliokuwa namba choo kwenye mkutano wa hadhara viwanja vya shule ya msingi Bomani alimuomba Waziri Biteko awafungulie Mgodi huo.
Shabani alisema tangu ufungwe wananchi na wachimbaji waliokuwa wamewekeza hapo wameshuka kiuchumi lakini pakifunguliwa wananchi watakuza uchumi wao kama ilivyokuwa awali.
Diwani wa Kata ya Katente Tabu Ng'hwani aliomba serikali ione umuhimu wa kufungua mgodi huo ili wachimbaji wafanye shughuli za kuchimba dhahabu ili walipe mapato ya serikali ambayo yatasukuma maendeleo ukiwemo ujenzi wa miudombinu ya Afya na Elimu
Taarifa nzuri, kikubwa wanaojiita wawekezaji waache janjajanja, ambao hatutaki adha watulipe tuwapishe wawendelee na uchimbaji
ReplyDelete