Wananchi wa Kijiji cha Busonzo-Bukombe wameiomba Serikali na wadau wa Maendeleo Kuwashika Mkono

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Busonzo.



Wananchi wa Kijiji cha Busonzo kwa umakini mkubwa wakimsikiliza Mbunge wao.




Wananchi wa Kijiji cha Busonzo Wilaya ya Bukombe Mkoani wa Geita, wameiomba serikali na wadau wa maendeleo kuwashika mkono ili kukamilisha ujenzi wa  Zahanati ambao mpaka sasa wamesgachangishana Tsh milioni 7 na jengo limefikia usawa wa madirisha.

Wito huo ulitolewa na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Busonzo Japhet Lubinza wakati akitoa changamoto za wananchi za kutembea umbali mrefu wa kufuata huduma za afya kwenye Kituo cha Afya Uyovu.

Lubinza alisema kutokana na changamoto hizo wananchi walinza Ujenzi wa Zahanati mwaka 2019 na walitarajia ujenzi ukamilike Juni 2021 ikiwa katika ujenzi huo  nguvu za wananchi sh 7 milioni hadi kukamirika mradi utagharimu sh 69 milioni.

Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko alichagia Tsh milioni 3 katika Ujenzi wa Zahanati hiyo.

Wakati akitoa fedha hizo Biteko aliwaomba wananchi wa Kata ya Busonzo kuendelea  na ushirikiano huo ili wakamilishe mradi huo haraka sambamba na kuibua miradi mingine mipya.  

Nae Diwani wa Kata ya Busonzo Safari Nikas  Mayala alimpongeza Mbunge kwa kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Busonzo.

"Tukiodoa Kijiji cha Busonzo Mbunge Biteko alishatushika mkono pia katika Ujenzi wa Zahanati ya ya kijiji cha Namparahala kwa kiwango kikubwa pamoja na Kijiji cha Nakayenze alitupa  saruji 90 na mabati 100 kijiji cha Nalusunguti"Alisema Safari.



Comments