Ilichokifanya Timu ya Mashabiki wa Simba kwenye Ufunguzi wa Doto Cup 2021







Timu ya Mashabiki wa Simba inayojiita Simba Fc ya Namonge Wilaya ya Bukombe Mkoani wa Geita, imetwaa zawadi ya msingi wa mchezo wa kufungua Ligi ya Doto Cup 2021 kwa kuichapa 3-0 Timu ya washabiki wa wa Yanga inayojiita Yanga Fc ya Namonge sekondari.


Mtanange huo umezikutanisha timu za watani hao Simba na Yanga za vijiji katika ufunguzi wa Ligi ya Doto Cup 2021 leo Julai 7, 2021 katika kiwanja cha Shule ya Sekondari Namonge.


Wafungaji wa magori ya Timu ya  Simba Fc kwa goli la kwanza lilifungwa na Balili Danifod dakika 8 goli la pili Juma Mhala dakika ya 32 goli na la tatu lilipachikwa nyavuni na Balili Danifod dakika ya 44.


Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Namonge na Mgeni Rasmi katika Ufunguzi huo Mlalu Bundala amekabidhi kitita cha Tsh 100, 000 kwa timu ya Mashabiki wa Simba huku timu ya Mashabiki wa Yanga wakikabidhiwa Tsh 50, 000.


Mlalu alisema lengo la Ligi hii ni kuibua vipaji kwa vijana hivyo vijana wacheze wakijuwa  kuwa michezo ni ajira na huimarisha afya pamoja na urafiki.


Nae  Mratibu wa Ligi ya Doto Cup 2021 Bosco Mwidadi alisema licha ya mechi hiyo ya kirafiki ya mashabiki wa Simba na Yanga katika ligi hii timu ambazo zimejipanga kushiriki ni  timu 156.


 "Timu zote zitaanza kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali vya kata zote 17 za Wilaya ya Bukombe kuanzia Julai 10, 2021" Alisema Mwidadi.


Comments