Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Yusuph Mohamed aliwaomba wataalamu kushirikiana na Madiwani wanapo kuwa wamefika kwenye miradi ya maendeleo ili kuwaondolea sintofahamu na hofu ya kwa nini miradi haikamiliki huku fedha zipo.
Mohamed ametoa ushauri huo leo Juni 9, 2021 kwenye Baraza la Madiwani wakati akijitimisha hoja ya kwa nini fedha zipo lakini hazijapelekwa kwenye miradi.
Nae Diwani wa Viti Maalumu Pili Kondela akichagia hoja hiyo alisema kuna fedha Tsh milioni 34 zimeshindwa kutumika kwa muda mrefu kwenye mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kagwe ambapo wananchi wanaendelea kufuata huduma za Afya maeneo ya jirani.
Aidha Afisa Mipango Wilaya ya Bukombe Wilbert Mtessigwa aliwaambia Madiwani kuwa fedha hizo za CSR toka Mgodi wa GGM na zimesha tumika kwa asilimia 96
Mtessigwa aliwaondoa shaka Madiwani huku akiwakumbusha kuwa kikao hiki ni kota ya tatu yani taarifa hizi zilitakiwa zijadiliwe mwisho Machi 30, 2021.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Dionis Myinga amewaomba Madiwani wa Halmashauri hiyo kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu kwa kuchangia nguvu zao kwenye miradi ya maendeleo ili kuondoa changamoto ya fedha zilizo tengwa kuishiwa munda na kurudishwa hadhina.
Comments
Post a Comment