Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisalimiana na Maafisa wa TFS.
(Watatu kutoka kushoto) Afisa nyuki Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita Daftoza Shayo akimuonyesha mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata asali kilichopo Kata ya Katente Wilayani hapa Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Damas Ndumbaro (wa pili kutoka kushoto huku wa kwanza kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe pia Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko wakiwa na Maafisa mbali mbali wa Wizara ya Maliasili na Utalii na halimashauri ya Wilaya ya Bukombe.
Wananchi pamoja na wafugaji nyuki wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Damas Ndumbaro wakati akizungumzia mikakati ya serikali kuwasaidia wafuga nyuki na taratibu za kutenga mapori ya hifadhi .
Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisistiza jambo kwa wananchi na watu wema wa Bukombe kabla ya kumkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Damas Ndumbaro kwenye mkutano wa hadhara.
(Wasaba kutoka kushoto) Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Damas Ndumbaro akitamburisha Maafisa wa Wizara yake pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Mary Masanja (wa pili kutoka kulia).
Waziri wa Maliasili na utalii Dk Damas Ndumbaro amemaliza hofu ya wafugaji wa nyuki ambayo ilikuwa imewatanda tangu hifadhi ya poli la Akiba la Kigosi Muyowosi kupanda hadhi kuwa National Park na kusimamiwa na Tanapa huku wakiambiwa wafuga nyuki waodoe mizingi yao kabla ya Julai 2021.
"Kuazia leo Juni 6, 2021 wafugaji wa nyuki kupitia vikundi
waendelee kufugia nyuki ndani ya hifadhi hiyo na watapewa kila kikundi maeneo ya kufugia"Dk Ndumbaro alisema.
Dk ndumbaro alisema serikali imefikia hatua hiyo baada ya Mbunge wa Jimbo la
Bukombe Mhe Doto Biteko kuifikisha changamoto hiyo ya wafuga nyuki aliomba wafugaji
wa nyuki waliokuwa wanafugia nyuki Kigosi Muyowosi waendele.
Alisema licha ya Serikali kipokea ombi la Mbunge Biteko wafugaji wafugie humo bila kuvunja sheria ya Uhifadhi na Serikali kupitia umuhimu wa uzalishaji wa asali bora Bukombe Wizara ya Mali yasili na utali iliamua kuwaletea Kiwanda cha kichakata
asali Bukombe.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba alisema Wilaya ya Bukombe inavikundi vya wafuga nyuki 38 vyenye wafugaji nyuki 1177 huku mizinga ya asili ikiwa 3698 na mizinga ya kisasa 6297.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko aliishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuwajengea Kiwanda cha kuchakata asali ili kuiongezea thamani hali ambayo itawafanaya kuwarahisishia masoko na kuuza kwa bei nzuri itakayo wafanya kuongeza kipato cha familia na Taifa kwa Ujumla.
Mwenyekiti
wa wafuga nyuki Wilaya ya Bukombe Emmanuel Maganga alisema wanaishukru serikali
kwa kuwaondolea hofu wafuga nyuki kutokana na hifadhi ya serikali kuu
kupandishwa hadhi na kusimamiwa na Tanapa huku wakiambiwa ifikapo Julai 1, 2021
wawe wameondoa mizinga na haitakiwi kuonekana ndani ya hifadhi ya Kigosi
Muyowosi.
Comments
Post a Comment