MWENYEKITI WA CCM MKOA WA GEITA AHIMIZA MIRADI IKAMILIKE KWA WAKATI

Muonekano wa Jengo la Baba Mama na Mtoto lililopo katika Kituo cha Afya Namonge

Hatua iliyofikiwa ya Jengo la Maabara ililopo katika Kituo cha Afya Namonge



 
Tenki la Maji Kijiji cha Buganzu lenye ujazo wa  lita 45,000, Mradi huo umegharimu Tsh milioni 158 kwenye Ujenzi wa Chanzo,Umeme na Pampu,vituo vinne vya Chotea Maji na mtandao wa Mabomba  

Baadhi ya Samani zinazotengenezwa na Kikundi cha Amani-Msonga baada ya kukopeshwa Tsh milioni nne kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe 



Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita Al haji Kalidushi  ameangiza Uongozi wa Halmashauri Wilaya ya Bukombe kukamilisha miundombinu ya Kituo cha Afya Namonge ili kianze kutoa huduma kwa wananchi kikamilifu.

Kalidushi alitoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa ya Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Namonge Dk Emmanuel Mrutu wakati akitoa taarifa ya mradi na changamoto zinazo pelekea kutotoa huduma kwa akinamama wajawazito.

Awali Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Namonge Dk Emmanuel Mrutu akitoa taarifa alisema  kutokana na changamoto hizo ambapo mradi ugekuwa umekamirika wagenufaika watu zaidi ya 41,147 wa Kata ya Namonge kwa kuwapuguzia kutembea umbari mrefu wa kufuata huduma za Afya katika Kata ya Uyovu hali ambayo ingepunguza vifo vya mama na mtoto.

Dk Mrutu alisema mradi wa ujenzi wa Zahanati uliazishwa kwa nguvu za wananchi 2012 kwa kuchagishana  sh 4.3 milioni na uongozi wa serikali ya kijiji ulitoa eneo la ukubwa wa hekari sita.

Alisema ilikuwa watumie Tsh milioni 53.2 na baada ya kupanda hadhi kuwa kituo cha Afya hadi sasa wametumia Tsh. milioni 90.5 ikiwa kati ya fedha hiyo Tsh milioni 5  kutoka Mfuko wa Jimbo na Mhe Biteko Tsh milioni 6,280,000 pamoja na Serikali kuu Tsh milioni 200. 

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Geita Rahel Ndegeleke akichagia maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa alishauri kuwa viongozi wa Halmashauri waanze kwa kutumia Tsh milioni 2.9  iliyotajwa kama baki  na ianze kwa kujenga shimo la kutupia kondo na la kuchomea taka  nakuacha kusubilia serikali ilete fedha huku kinamama wajawazito wakiendelea kuteseka kufuata huduma kwenye Kata jirani.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba  alisema  kwa kushirikiana na Wataalamu wa Halmashauri pamoja na Madiwani watatekeleza  maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa kwenye miradi nane iliyokaguliwa na Kamati ya Siasa Mkoa.

Comments