Wanafunzi wa Katome Sekondari Watoa Shukrani zao

 



Wanafunzi 111 wa Shule ya Katome Sekondari iliyopo Kata ya Katome Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita.wameishukru serikali na wazazi wao kwa kuwajengea shule karibu na kuwaondolea changamoto ya kutembea umbari mrefu wa kilomita 30 kwenda na kurudi huku wengine wakitembea hadi kilomita 40 kwenda na kurudi Butinzya Sekondari.


Wameyasema hayo shuleni hapo wanafunzi Jenipha Paul na Amos Deogoratius wakizungumza na blog ya Bukombesasa kwa nyakati tofauti wakiishukru serikali kwa kushirikiana na wazazi kujenga shule karibu na mazingira wanayoishi hali ambayo imewaodolea adha ya kutembea umbari mrefu.


Paul alisema kabla ya shule kujengwa walikuwa wanakutana na changamoto ya vishawishi vingi vya wanaume njiani na wengine waliacha shule kwa kubebeshwa mimba na wengine wakipata mdondoko wa kitaluma.


Nae Deogratius alisema walikuwa wanachelewa kufika nyumbani kutokana na kutembea umbari mrefu walifika wamechoka hali ambayo ilikuwa inapelekea kushindwa kutenga muda wa kujisomea hivyo kujengwa shule karibu inawasaidia kuondokana na gharama ya kupanga chumba walikuwa wanalipia Tsh 10,000 kwa mwezi badala yake pesa hiyo watanunuliwa mahitaji mengine.


Kwa upande wake Kaimu mkuu wa shule ya Katome Sekondari Frolian Bernard alisema

ujezi ulianza 2017 kwa lengo la kuwapunguzia changamoto ya kutembea umbari mrefu wanafunzi  walikuwa wanalazimika kutembea kilomita 30 kwenda na kurudi  wakitokea Katome kwenda Butinzya Sekondari.


Nguvu za wananchi  sh milioni 22. 6  na  Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko alichangia Tsh 11 zilizonunua mabati 265  mifuko ya simenti 300 huku halmashauri iliongeza sh 5,569.68 na vifaa vya ukamirishaji vyumba vya madarasa matano vilitolewa na mgodi wa GGM, mifuko ya saruji 20  mbao 460 na sh 300, 000 zilitolewa na mkuu wa wilaya Said Nkumba.


Shule ilifunguliwa Machi 15, 2021 kwa namba za usajiri S5533  kwa uhitaji mkubwa wanafunzi walikuwa wanatembea umbari mrefu  kwenda Butinzya sekondari kutoka Katome kilomita 15 hadi 20 shule imeanza na  wanafunzi 111 wavulana 47 wasichana64


Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Bukombe Philibert Nyagahondi alisema hadi 2020 wilaya ina kata 17 shule za sekondari zilikuwa 15 lakini mwaka huu wamefungua shule mbili ambazo ni Dotobiteko Sekondari Kata ya Igulwa na Katome Sekondari na kufikisha shule 17 ili kuwaondolea wanafunzi changamoto na vishawishi vinavyo sababishwa na kutembea umbali mrefu.


Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba alitoa wito kwa wadau wa elimu kuendelea kusapoti nguvu za wananchi kwa kuchagia mali zao katika miradi ya maendeleo

Comments