MADIWANI HAMASISHENI WANANCHI KUCHANGIA NGUVU ZAO KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

Waheshimiwa Madiwani wakifuatilia taarifa za miradi ya maendeleo kwenye makabrasha


 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukombe Mkoani Geita Yusuph Mohamed amewaomba Madiwani kuendelea kuhamasisha wananchi kuendelea kuchagia nguvu zao katika miradi ya maendeleo bila kusahau uibuaji wa miradi mipya.

Mohamed ametoa wito huo leo Machi 30, 2021 kwenye kikao cha madiwani  ambapo Diwani wa kata ya Bulenga  Erick Kagoma amesema wananchi uchagiaji unaeda taratibu sana.

Kagoma amesema utekelezaji wa miradi ya maendeleo ujenzi wa bweni la wasichana katika shule hiyo liko katika hatua ya mwisho wanapaua ameiomba Serikali kuleta fedha za vitanda na magodolo ya bweni hilo.

Amesema Shule ya Sekondari Bulenga inauhitaji wa vyumba vya madarasa 22 huku yaliyopo ni 9 na upungufu ni 13 pia alieleza wananchi wamesha jenga madarasa manne  yako usawa wa renta na mengune yakiwa usawa wa madirisha,

Kagoma amesema wananchi wa  Kata ya Bulenga kwa nguvu zao wametengeneza  viti  na Meza138  tayari meza 22 zimekamilika na wanatarajia kutumia  kiasi cha Tsh. milioni 2.9 ikiwa ni nguvu za wananchi. 


Pia Kagoma ametoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambae pia ni Waziri wa Madini Doto Biteko kwa kuwashika mkono wananchi kwa kuchangia mabati 220 ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Bulenga yaliyogharimu zaidi ya milioni 6.

Comments