Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita Mhe Doto Mashaka Biteko ameamua kuipiga jeki kata ambayo imebaki nyuma
bila kuwa na shule ya sekondari kati ya
kata 17 ambayo nikata ya Nganzo kutokana na wananchi wa ke kubweteka wakisubiri
wadau na serikali.
Biteko alifikia hatua hiyo baada ya kufika
kwenye Kata hiyo ambapo alikuta ujenzi unachelea na kuendelea kuwafanya
wanafunzi kwenda Kata jirani ya
Bulenga na wengine kwenda Sekondari ya Butinzya
Biteko akiwa kwenye majengo ya madarasa na
kuona hali halisi ya changamoto hiyo ya ukamirishaji wa vyumba vinne na vya madarasa Ofisi moja na
kuchangia zaidi ya Milioni 9 kwa ajili
ya mabati 240 ya kuezekea na gharama za ufundi na misumari
“Wana Bukombe wenzangu tuongeze nguvu
katika utekelezaji wa miradi ili tuwe na Bukombe itakayokutwa na vizazi vyetu
vijavyo ikiwa katika hali nzuri kimaendeleo”alisema Mhe Biteko
Miongoni mwa Wadau wa Maendeleo wa Wilaya
Bukombe Gungu Nsangari aliungana na Mbunge kwa kuchangia mbao zenye thamani y
ash 4.5 milioni ambapo Katibu wa CCM Wilaya Bukombe Josephat Chacha alipongeza
jitihada za Mbunge Biteko kwa kuendelea
kuwahamasisha wananchi kuchangia maendeleo.
Comments
Post a Comment