WAZIRI WA MADINI AZITAKA KAMPUNI ZA UTAFUTAJI WA MADINI KUENDELEZA MAENEO YA LESENI ZAO




Waziri wa Madini, Doto Biteko amezitaka kampuni za utafutaji wa madini nchini kufanya shughuli za utafutaji wa madini, badala ya kuyatelekeza maeneo yao ya leseni,  vinginevyo leseni zao zitafutwa kwa mujibu wa sheria.


Waziri Biteko ameyasema hayo leo tarehe 21 Januari, 2021 kwenye kikao chake na kampuni ya uchimbaji wa madini ya Shanta Mining inayojihusisha na utafutaji na uchimbaji wa dhahabu katika maeneo ya Songwe na Singida.


Amesema kuwa ni vyema kampuni zinazopewa leseni za utafiti wa madini kuhakikisha zinaendeleza maeneo yao badala ya kuyaacha pasipo kuyaendeleza.





Wengine waliohudhuria katika kikao hicho ni pamoja na Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Madini, Edwin Igenge, Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Augustino Ollal, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba na Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini- Sehemu ya Uongezaji Thamani Madini, Bertha Luzabiko

Washiriki kutoka katika kampuni ya Shanta Mining walikuwa ni pamoja na Meneja Mkuu, Exupery Lyimo, Mkurugenzi wa Ufundi Honest Mrema, Meneja Mkuu-Mahusiano na Serikali, Mhandisi Philbert Rweyemamu na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu, Calvin Mlingi. 

Comments