Biteko Awawashia Taa Nyekundu Wanunuaji wa Madini kwa Njia za Magendo

 




 Waziri wa Madini Doto Biteko ametoa onyo kali kwa baadhi ya watu wasio waaminifu wanaojishughulisha na biashara ya madini kwa njia za magendo na kusema kuwa,

Wizara haitamvumilia yeyote atakayejihusisha na biashara hiyo kwa kuwa atakuwa anahujumu uchumi wa nchi kwa makusudi.


Waziri Biteko ameyasema hayo leo Januari 11 katika ziara yake ya kutembelea Soko la Madini jijini Dar es Salaam ambapo pia amekutana na wafanyabiashara wadogo wa madini mkoani humo.


Amesema 

kwa sasa Serikali imekwishatengeneza mazingira wezeshi katika biashara ya madini ili kuhakikisha madini ya Tanzania yanatambulika kitamataifa.


"Nawasihi wale wote wanaonunua madini majumbani kuacha mara moja, tutawafikia popote walipo na kuwachukulia hatua za kisheria kwa kuwa tumeshajizatiti kuyalinda madini na kuhakikisha yanawanufaisha watanzania wote.


Aidha, amewataka wafanyabiashara kutumia brokers ambao ni waaminifu ili kuhakikisha usalama wa fedha zao na kuwahakikishia ulinzi wale wote watakaokuwa tayari kufanya biashara kwa uwazi na uaminifu.


Naye, Naibu waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya amewaasa wafanya biashara hao kufichua waovu ili kutengeneza mazingira rafiki kati yao na Serikali na kuiwezesha kuwa chombo cha uwezeshaji badala ya udhibiti.



Kwa upande wake, Mwenyekiti waTume ya Madini Prof. Idris Kikula amewashauri wafanyabiashara hao kutoa vitambulisho kwa wafanyakazi waliowajiri katika ofisi zao ili waweze kutambulika katika ofisi mbalimbali.


 Waziri Dotto Biteko ameendelea na ziara ya kuwatembelea wanyabiashara wa madini na kusikiliza kero na changamoto zao na kutoa suluhisho la pamoja ili kuboresha biashara ya madini nchini.

Comments