WIZARA YA MADINI YAMPOKEA RASMI PROF.MANYA



Awashukuru Watumishi kwa ushirikiano

         



Aliyoyasema Waziri wa Madini, Doto Biteko

Tufurahie tujikua na kukumbuka tuna kazi kubwa mbele yetu za kufanya, kinachotakiwa kwetu kwa sasa ni matokeo, kama mnavyofahamu umuhimu wa sekta yetu kwa maendeleo ya nchi.


Nyumba yetu inafuraha sana, tumepata kiongozi ambaye ametoka miongoni mwetu, namshukuru sana Mungu kwa ajili yako, kama familia ya madini tunakupongeza sana.


Ukiona Mhe, Rais ambaye ana watu zaidi ya milioni 20 amekuchagua, ni kwasababu ya matokeo mazuri yaliyoonekana kwenye sekta ya Madini. Mafanikio haya si ya Manya ni kwenu nyote, nawapongeza sana kwa ushirikiano mliompatia ikapelekea kupata nafasi


Uchimbaji wa makaa ya mawe lazima uanze.


Aliyoyasema Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya


Sisemi kwamba ni kwasababu ya uelewa, vipaji, taranta wala maarifa bali wizara na taasisi zake hususan Tume ya Madini. Matokeo yenu mazuri yamenipa ngazi ya kupandia, yaliyofanyika kwenye Sekta ya Madini yanaonekana.


Mhe. Rais anatamani Sekta ya Madini kutoka hatua moja kwenda nyingine, tuendelee kufanyiakazi maono yake ili tujenge uchumi wa nchi yetu.



Nashukuru nipo kwenye jamii ya watu ninaowafahamu, nawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipatia kwa kipindi cha miaka mitatu ambayo tumefanya kazi pamoja, tuendelee kushirikiana ili Sekta ya Madini iendelee.



Naamini nitaendelea kuwa bora ili kuwa kiongozi niitumikie nafasi hii. Ubunge ni kitu ambacho sikuwahi kukiwaza, naamini kwa pamoja tutavuka.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon Msanjila.


Amekuja mwenzetu tunajuana, kama ni madaraka atajifunza, tunaahidi kuendelea kushirikiana. 

Comments