KAMPENI ZA CCM BUNTUBILI KATA YA IGULWA

Na Jonathan Samwel


Mgombea wa Udiwani  Kata ya Igulwa amewashukuru wananchi pamoja na Mheshimiwa Doto Mashaka Biteko kwa kufanikisha ujenzi wa Shule ya sekondari kwani Kata ya Igulwa ilikuwa na shule za msingi tano lakini hakukuwa na shule ya sekondari hivyo kusababisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari kutembbea umbali mrefu kufuata elimu pia amewashukuru wananchi  kwa kujitoa katika ujenzi wa Zahanati katika Kata ya Igulwa


Mgombea wa udiwani Kata yw Igulwa Simon charles Mabenga akiomba kura kwa wananchi wa kata ya Igulwa


Akiendelea na shukrani hizo Mabenga alisema Mhe. Doto Biteko  pia aliwashika mkono katika Ujenzi wa Zahanati  katika kata hiyo.


Nae Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko amewahakikishia wananchi wa Kata ya Igulwa kuwa serikali ya awamu ya tano imeshasambaza umeme katika kila makao makuu ya Kijiji na sasa kazi hiyo inaaendelea kupeleka umeme nyumba hadi nyumba. 


Biteko alisema  atakapochaguliwa kuwa Mbunge  atashirikiana na Wananchi

Comments