MLALU AMPIGIA SALUTI BITEKO KWA WAPIGA KURA



Mgombea wa udiwani CCM kata ya Namonge Mlalu Bundala akizungumza na wananchi wa kata ya Namonge







Mgombea Udiwani kwa Tiketi ya ChamaCha Mapinduzi Ccm Kata ya Namonge Mlalu Bundala alisema maendeleo ya Kata hiyo yameletwa na jitihada za Mbunge Biteko kwa kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dk John Pombe Magufuli.

Bundala alisema mwaka 2010 Kata ya Namonge ilikuwa inaletewa fedha za maendeleo chini ya Tsh milioni  100  kutokana na Diwani na Mbunge kupitia CHADEMA walikuwa hawahamasishi maendeleo kwa wananchi kushiriki kikamirifu lakini tangu 2015 hadi 2020 Serikali imeleta Tsh bilioni 3.5  za miradi ya maendeleo kutokana na wananchi kuhamasishwa na kuanza kuchagia miradi huku wakiibuwa miradi mingine mipya.


Kwa upande wake Mgombea Ubunge Jimbo la Bukombe Doto Biteko alimshukru Rais Dk John Pombe Magufuli kwa kazi aliyoifanya ya kutenga fedha za miradi hadi vijijini tangu 2015 hadi 2020 maendeleo yameonekana kata ya Namonge ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Afya, shule za msingi kuongezeka, Umeme kila kijiji na vitongoji vyake na kuongezeka mtandao wa barabara kutoka kilomita 25 hadi 60 .

Biteko alitoa pongezi hiyo wakati akielezea Maendeleo ya Kata ya Namoange wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni zake za kusaka Ubunge.

Biteko aliwaomba wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli na diwani Mlalu  Bundala ili katika nafasi ya Ubunge 2020 hadi 2025 Bukombe iwe na mabadiliko katika maendeleo.

Comments