Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula (MB) ameitaka halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kutoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari na mikutano ya hadhara juu ya sheria Na 8 ya fedha ya mwaka 2020 ya umiliki wa ardhi. Sheria hiyo ilianza kutekelezwa tarehe 1 Julai 2020 inayowataka wananchi kumilikishwa ardhi ndani ya siku 90 baada ya mchoro kuwa umeidhinishwa vinginevyo watakutana na limbikizo la kodi.
“wananchi wapewe elimu juu ya sheria mpya inayowataka wananchi ambao maeneo yao yalishapimwa na kidhinishwa kuomba umiliki wa viwanja vyao.”
Mabula ameyasema hayo leo tarehe 12 Agosti, 2020 wakati wa ziara yake Wilayani Bukombe.
Aidha ameitaka Idara ya Ardhi kuhakikisha inapima maeneo yote ya Umma kama masoko, vituo vya polisi, stendi, ofisi za zima moto, hospital, shule na maeneo mengine ambayo ni mali ya Umma ili kuepusha migogoro.
“Lazima maeneo yote ya Umma yawe yamepimwa na yamemilikishwa ili kuepusha migogoro ya taasisi na wananchi.”
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Said Nkumba amesema Idara ya Adhi inachangamoto ya upungu wa watumishi katika kada za Afisa Ardhi Mteule 1, Mtunza kumbukumbu 1, Maafisa Mipango Miji 2, Mrasimu Ramani 1 na Wathamini 2. Hata hivyo halmashauri kupitia Ofisi ya Utumishi inaendelea kuomba vibali vya kuajiri watumishi hao.
Kwa upande wake Afisa kilimo Umwagiliaji na Ushirika Wilaya (DAICO) Joseph Machibya kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji amesema Halmashauri iliwekewa lengo la kukusanya jumla ya shilingi 300,000,000.00 kutokana na tozo mbalimbali za ardhi. Hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2020 halmashauri ilifanikiwa kukusanya jumla ya shilingi 110,547,997.00 sawa na asilimia 36.67 ya lengo. Aidha changamoto kubwa iliyopelekea kutofikia ni kutokuwa na watumishi wakutosha pamoja na vitendea kazi.
Hata hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ilipokea fedha kiasi cha shilingi 123, 000,000.00 kutoka wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya upimaji wa viwanja 2,000 katika maeneo ya Msimila na Uyovu. Hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2020 jumla ya viwanja 2,672 vimemepimwa sawa na asilimia 133.6 ya lengo.
Regina Ndungulu akipokea hati ya umiliki wa Ardhi kutoka kwa Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula.
Baadhi ya washiriki wa kikao
Wananchi wakiwa wameshikilia hati miliki nyuma ya Naibu waziri wa Ardhi.
Comments
Post a Comment