NYUMBA YA MFANYABIASHARA YATEKETEA KWA MOTO


Nyumba ya makazi inayomilikiwa na mfanyabiashara wa nguo Mwita Jackson maarufu Mwita Sound imeteketea kwa moto mtaa wa Katente Wilaya ya Bukombe mkoani Geita huku chanzo kikidaiwa ni kulipuka kwa Genereter iliyokuwa imehifadhiwa ndani ya nyumba hiyo.

 

Akizungumza Jackson nyumbani kwake na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba na Waziri wa Madini Doto Biteko alisema akiwa kwenye majukumu yake majira ya saa 6 mchana Julai 08 mwaka huu alijulishwa kupitia simu kuwa nyumba inateketea kwa moto na alipofika alikuta nyumba na baadhi ya vitu vya thamani vimeteketea licha ya majirani kuonyesha jitihada kubwa za uokoaji.

Kwa upande wake Waziri wa Madini Doto Biteko alimpa pole mfanyabiashara huyo kwa kupatwa na tukio hilo la nyumba ya makazi na kwamba alimshukru Mungu kuinusulu familia na janga hilo.

“Nawashukuru sana wananchi wenzangu kwa ushirikiano mliouonyesha kwa ndugu yetu Mwita hii ni hali ya kuonyesha ushirikiano wa dhati kabisa kwani matatizo yako kwa kila mmoja wetu” Alisema Biteko.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Said Nkumba alitoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kuweka vitu vinavyoweza kulipuka ndani ya nyuma wanazoishi badala yake wawake sehemu ambazo hazitaingiliana na shunguli za kifamilia.

Nkumba alisema tukio hilo bado polisi wanachunguza ili kujua chanzo cha athari iliyo mkuta wananchi huyo ili thamani ya nyumba na vifaa itolewe na kwamba wananchi wajihadhali na matumizi ya mafuta ya petrol kwenye kufua nishati ya umeme kwa kutumia Genereter ili kuepuka mathara ambayo sio ya lazima.

MWISHO


Comments