WIZARA YA MADINI YAJIVUNIA KUVUKA LENGO LA UKUSANYAJI KODI



 Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko amewataka wachimbaji wadogo wadogo na wakubwa kuendelea kuwa waminifu kulipa tozo za serikali na kuacha tabia za kutorosha madini hali ambayo imeifanya Wizara hiyo kuvuka lengo la ukusanyaji kodi.
" Mei 31 mwaka huu Wizara imekusanya tsh bilioni 479.9  huku serikali iliipangia Wizara kukusanya Tsh bilioni 470.3  ifikapo Juni 30 mwaka huu nna imani Wizara itakusanya tsh bilioni 500 " Alisema Biteko.
 

 Biteko aliyasema hayo wakati akizungumuza na wachimbaji wachimbaji wadogo na wakubwa wa madini ya dhahabu kwenye soko la dhahabu mjini Geita wakati wa ziara yake ya kwenda kukaguwa ujenzi jengo jipya la soko lililojengwa kutokana na fedha za Uwajibikaji wa migodi kwa jamii (CSR) zinazo changiwa na mgodi wa GGM.
 
Aidha Biteko alikemea tozo zisizo za lazima kwa wachimbaji wadogo wadogo zinazo tozwa na baadhi ya wamiliki wa Leseni na serikali za vijiji huku serikali ilishaondoa tozo zingine zisizo za lazima ili kuepusha utoroshwaji wa madini.


Pia Biteko alisema Wizara imesimamia vizuri wachimbaji wadogo licha ya kuwepo changamoto za ukusanyaji wa kodi mwaka huu kutokana na kushuka kwa uzarishaji kutokana na Mvua nyingi pamoja na janga la Corona.


Kwa upande Mkuu wa Mkoa wa Geita Robart Gabriel alisema kupitia sekta ya madini kuna mabadiliko makubwa ya maendeleo mkoani Geita ikiwa huduma mbali mbali za kijamii zinaboreshwa hasa huduma za Afya, Elimu na masoko ya kisasa kwa ajili ya wananchi wa kipato cha chini.


Nae Makamu wa Rais wa Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM) Simon Shayo  alisema wamejipanga kuhudumia jamii kwa kujenga soko la wajasiliamali hali ambayo itapandisha kipato kwa akinamama na wametenga sh 5.5 bilioni kwa ajili ya huduma za kijamii likiwemo soko la wajasiliamali na dhahabu.






Comments