Baadhi ya wana CCM waliojitokeza kujaza fomu za kumdhamini Rais Dkt.
John Pombe Magufuli ili aweze kuteuliwa kugombea tena nafasi ya urais
katika uchaguzi ujao. Waziri Mkuu na Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa
aliongoza zoezi hilo kwenye Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo, Juni 21,2020.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati mwanachama wa CCM, Jacob
Masumbuko alipotia saini fomu ya kumdhamini, Rais Dkt. John Pombe
Magufuli ili aweze kuteuliwa kuteuliwa tena kugombea urais. Zoezi hilo
lilifanyika kwenye Ofisi ya CCM ya wilaya ya Rungwa, Juni 21, 2020.
Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa LIndi, Fadhili Juma.(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Makuu, Kasim Majaliwa akishuhudia wakati wana CCM walipojitokeza
kujaza fomu za kumdhamini Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze
kuteuliwa tena kugombea urais katika uchaguzi ujao. Wa pili kulia ni
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi , Fadhili Juma. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Makuu, Kasim Majaliwa akishuhudia wakati wana CCM walipojitokeza
kujaza fomu za kumdhamini Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze
kuteuliwa tena kugombea urais katika uchaguzi ujao. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi , Fadhili Juma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa ameongoza wanachama 314 wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) wilayani Ruangwa, Lindi katika kujaza fomu za kumdhamini Rais Dkt.
John Pombe Magufuli ili aweze kuteuliwa kugombea tena nafasi ya urais.
Idadi hiyo
inafanya jumla ya wanachama waliojitokeza kumdhamini Rais Dkt. Magufuli
katika wilaya hiyo kufikia 2,565 baada ya wanachama wengine 2,251 kujaza
fomu hizo jana (Jumamosi, Juni 20, 2020) na kumdhamini kiongozi huyo.
Waziri Mkuu
ameongoza wanachama hao wa CCM leo (Jumapili, Juni 21, 2020) katika
ofisi za CCM wilayani Ruangwa. Amewasihi wananchi hao waendelee kuwa na
imani na Rais Dkt. Magufuli pamoja na Serikali anayoiongoza.
“Mheshimiwa
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametekeleza ahadi zote alizoziahidi
ikiwemo ya kuwatumikia Watanzania wote hasa wanyonge. Amewatumikia
Watanzania wote bila ya kujali itikadi zao za kisiasa na hata za kidini.
Nawapongeza wana CCM wenzangu mliojitokeza kumdhamini rais wetu.”
Waziri Mkuu
ameongeza kuwa “Kitendo mlichokifanya leo kinaonyesha shukrani kubwa
kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye wakati wote
ameonesha mapenzi makubwa kwetu pamoja na Watanzania wote kwa ujumla.”
Amesema kwa
sasa wilaya ya Ruangwa imepata mabadiliko makubwa kimaendeleo ambayo
hapo awali hayakuwepo kama nishati ya umeme, maji ambayo kwa sasa kila
kijiji kina kisima, shule za msingi katika kila kijiji na sekondari
kwenye kata zote pamoja na barabara za lami katika mitaa ya mji wa
Ruangwa.” Haya yote ni Dkt. Mgufuli.”
Kwa uapande wake,
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi, Fadhili Juma amesema wanaCCM wa mkoa
huo wapo bega kwa bega na Rais Dkt. Magufuli na kwamba watahakikisha
anapata kura nyingi katika uchaguzi ujao.
Awali,
Waziri Mkuu aliwashukuru WanaRuangwa wote kwa ushirikiano waliompatia
katika kipindi chote cha miaka mitano ambao ulimuwezesha kutekeleza
majukumu yake ya kuwaletea maendeleo kwa ufanisi mkubwa.
Comments
Post a Comment