TAKUKURU YAWAKAMATA VIGOGO WA ZAMANI MSD


Aliyekuwa mtendaji mkuu wa MSD Nchini Laurian Bwanakuru amekamatwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU )makao makuu ..
Taarifa ya Takukuru iliyotolewa leo inasema kuwa mbali ya mkurugenzi huyu yupo pia kaimu mkurugenzi wa Lojistiki  wa MSD Byekweso Tabura ambao kwa pamoja wanashikiliwa mahabusu katika ofisi ya TAKUKURU Upanga jijini Dar es  Salaam .
Taarifa iliyotolewa na ofisi mahusiano wa TAKUKURU Doreen Kapwani inadai kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kuhusika na matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kuisababishia hasara serikali kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007

Comments