MCHIMBAJI WA DHAHABU JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA MWANAFUNZI DARASA LA KWANZA

Infections And Incarceration: Why Jails And Prisons Need To ...
Mahakama ya wilaya ya Bukombe mkoa wa Geita imemtia hatiani mkazi wa kijiji cha Nyakafulu aliyekuwa mchimbaji wa madini ya dhahabu kijijini hapo Ruben Misanga (47) kwenda kutumikia adhabu ya mika 30 jela baada ya kumkuta na hatia ya kubaka mtoto wakike mwenye umri wa miaka (10) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Nyakafulu.
Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Bukombe Mjuni Mchunguzi akisoma hukumu kwa mshtakiwa alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo la kubaka Septemba 8 mwaka 2019 muda ambao haukujulikana  nyumbani kwake akiishi na mtoto huyo wa kike akiwa amemfanya mke wake.

Mchunguzi alisema kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haujaacha shaka, mahakama inamtia hatiani mshtakiwa  kwenda jela miaka 30 ili liwe fudisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Awali mwendesha mashtaka wa polisi wilaya ya Mbogwe Rashid Kitabu  aliiambia mahakama kuwa matukio ya unyanyasaji kwa watoto wadogo wa kike migodini yamekisiri na yanazidi kuongezeka.

Kitabu aliomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa huyo ili kukomesha unyanyasaji na ukatili kwa watoto wakike migodini.
Mshtakiwa alipewa nafasi ya kujitetea hakujitetea chochote ndipo mahakama ikaamulu mshtakiwa kwenda jela miaka 30.


Comments